Mwanamuziki wa Bongo Flava na mmiliki wa Lebo ya Konde Gang Rajab Kahali maarufu Harmonize, kupitia ukurasa wake wa instagram ameeleza kusikitishwa na maneno ya uzushi yanayoendelea kuhusu yeye na mwanamuziki Anjella.
Amesema kama kuna mtu anayeweza kujitokeza na kutaka kumuendeleza mwanamuziki huyo ruksa, kwani anachotaka yeye ni kumuona anafika mbali zaidi.
“Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu najua kuna wenye uwezo mkubwa kunizidi ukizingatia nimeanza juzi, kama kuna anayeweza kumuendeleza kipaji chake ni faraja kwangu na asisite kujitokeza, PUUZIA SIASA ZA KUSEMA SIJUI NAMDAI MAHELA, SIJAWAHI KUTAKA HATA SENTI MOJA.” ameandika Harmonize
Anjella ni mwanamuziki wa kike wa kwanza kusainiwa na lebo hiyo na bado ana uhusiano mazuri na Harmonize kwa maelezo ya mmiliki huyo wa Lebo ya Konde Gang.