Filamu ya Kitanzania, ‘Still Okay To Date?’ imeshinda Tuzo za Kalasha zinazoandaliwa na Bodi ya Filamu ya Kenya.
Filamu hiyo imenyakua tuzo katika kipengele cha Filamu Bora za Kimataifa (Best International Award) kilichoshindanisha filamu kutoka nje ya Kenya ikiwemo filamu kutoka Uganda na nyingine tatu kutoka Tanzania.
Watozi wa Filamu hii ni Kefa Igilo (@kefa_ig) mtozi wa vipindi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akishirikiana na Jerryson Onasaa (@code_Jerry) na ndio ambao wamepokea tuzo hiyo.