EPL kuendelea usiku wa leo

0
184

Timu ya Arsenal inashuka dimbani hii leo dhidi ya Southampton katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Arsenal ipo nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu England, hivyo inahitaji ushindi katika mechi ya leo ili kuendelea kujiweka vizuri katika msimamo wa ligi hiyo

Mabingwa watetezi Liverpool watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya vinara wa ligi hiyo Tottenham Hotspur watakapowakaribisha katika dimba la Anfield.

Katika mechi nyingine, Leicester wanaoshika nafasi ya 3 katika ligi hiyo watashuka dimbani dhidi ya Everton huku West ham United wakicheza dhidi ya Crystal Palace, Leeds United wakichuana na Newcastle United na Fulham dhidi ya Brighton & Hove Albion.