Dkt. Abbasi aungana na wasanii kuwaburudisha waliohudhuria Tamasha la Bagamoyo

0
3271

Wasanii wa Bongo Fleva na Muziki wa Taarabu wanakiwasha katika Tamasha la 40 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni lililozinduliwa leo Oktoba 29, 2021 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa katika viwanja vya TaSuBa, Bagamoyo.

Wasanii hao wamewakosha wadau mbalimbali na viongozi kwa kipaji chao cha kuimba na kucheza.

Hali iliyopelekea kuwanyanyua baadhi ya viongozi waliohudhuria tamasha hilo akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi ambaye pia alionesha umahiri wake wa kucheza na kuchana mistari.

Ikumbukwe kuwa wakati akiwatambulisha wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha hilo kwa Waandishi wa Habari Oktoba 26, 2021 Dkt. Abbasi alisema katika Tamasha hili ataongoza wasanii wa Hiphop kuchana mistari

Wasanii waliotumbuiza ni pamoja na Beka Flavour, Isha Mashauzi, Saada Nassor, Saraphina na Ruby.

Tamasha hilo linaendelea na linatarajiwa kufikia kilele hapo kesho Oktoba 30, 2021.