Diamond atunukiwa Tuzo ya heshima kwa kueneza Kiswahili

0
1925

Taasisi moja ya Kiswahili ya nchini Canada imemtunuku Tuzo ya heshima Msanii nyota wa Muziki wa Tanzania Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond Platnumz, kutokana na kutambua mchango wake katika kueneza lugha ya Kiswahili.

Taasisi hiyo ya Swahili Vision International Association (SVIA), imemtunuku Diamond Tuzo hiyo kutokana na mchango wake ambao amekua akiutoa katika kueneza lugha ya Kiswahili Kimataifa kupitia Muziki wake.

Tuzo hiyo pia imetolewa kwa Kampuni ya Wasafi, ambayo inamiliki Lebo ya Muziki ya Wasafi.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, Meneja wa Diamond, -Babu Tale amempongeza Diamond kwa kutunukiwa Tuzo hiyo ya heshima na kumtaka aongeze juhudi katika kuitangaza lugha ya Kiswahili pamoja na nchi ya Tanzania kupitia Muziki wake.