Diamond ang’ara Afrika

0
1807

Msanii NASEEB Abdul Maarufu kama Diamond Platnumz ametajwa kwenye orodha ya wasanii 10 wakubwa zaidi Barani Afrika

Kwenye Orodha iliyotajwa na Shirika la Habari CNN pia wametajwa ‘African Giants’ wengine kama Burna Boy, Davido, Wizkid, Yemi Alade, Tiwa Savage, Mr Eazi, Sho Madjozi, Busiswa Gqulu na Slapdee

Diamond Platnumz ametajwa kwenye orodha hiyo kufuatia Ukubwa wa nyimbo zake na alizoshirikishwa pamoja na Matamasha aliyoyafanya na Tuzo mbalimbali alizowahi kushinda huku wakitolea mfano Tuzo za MTV EMA za Mwaka 2015 ambapo Diamond aliweka rekodi kwa kuwa masanii wa kwanza Afrika kushinda tuzo hizo mbili ndani ya Usiku Mmoja.