Davido aongeza msanii mpya

0
1130

Staa wa muziki kutoka Nigeria, Davido, kupitia lebo yake ya Davido Music Worldwide (DMW) ameongeza ladha ya burudani kwa kumsaini msanii mpya.

Davido ambaye anazidi kukuza lebo yake siku hadi siku, amethibitisha taarifa hizo kupitia insta story yake baada ya kufanikiwa kumsaini AyanFe kupitia lebo yake hiyo.

DMW ina jumla ya wasanii 8 akiwemo: Mayorkun, Dremo, Ichaba, Yonda, Perruzi, DJ ECool, Idowest na sasa AyanFe.