Corona yamzuia Diamond kufanya shoo majuu

0
1605

Shoo za mwamamuziki wa Tanzania, – Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, zilizopangwa kufanyika katika nchi mbalimbali barani Ulaya zimesitishwa kutokana na tishio la virusi vya corona ambavyo vimeenea katika baadhi ya nchi za bara hilo.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa  kijamii wa Instagram, Diamond ametoa taarifa ya kusitishwa kwa shoo hizo na kuongeza kuwa zitapangwa tena katika siku za baadae.

Diamond alipanga kufanya shoo katika nchi za Ubelgiji, Ufaransa, Ujerumani, Finland na Sweden kuanzia Machi 13 hadi Aprili nne mwaka huu.