Chynna afariki akiwa na miaka 25

0
2585

Rapa na mwanamitindo Chynna Rogers maarufu kwa jina la Chynna amefariki dunia leo nyumbani kwake Philadelphia, Marekani akiwa na miaka 25.

John Miller ambaye ni meneja wake Chynna amethibitisha taarifa za kifo rapa huyo na kusema sababu ya kifo chake bado haijajulikana.

Kifo cha nyota huyu kimekuja miezi minne tu baada ya kuachilia ‘Extended Play (EP)’ inayokwenda kwa jina la “If I Die First.”

Chynna alianza kazi ya mitindo akiwa na miaka 14 baada ya kusainiwa na Ford Models.