Billnass na Nandy wafunga pingu za maisha

0
3371

Mastaa wawili wa muziki Tanzania, William Lyimo (Billnass) na Faustina Mfinanga (Nandy) wamefunga ndoa leo katika kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Beach na kuyahalalisha mahusiano yao yaliyodumu kwamuda mrefu sasa.

Mapema wiki hii Nandy alifanyiwa sherehe kubwa mbili ya Kitchen Party na Send-off akiwa katika mionekano tofauti tofauti.

Katika interview moja, alipoulizwa kuhusu kusogeza mbele siku ya ndoa yake, Nandy ambaye ana mimba kubwa akisogelea siku za kujifungua alisema kuwa moja kati ya jambo alilokuwa akipendelea sana ni kujifungua mtoto akiwa kwenye ndoa na hivyo ujauzito wake hautozuia ndoa yake kufungwa kama ilivyopangwa.

Akiwasili kanisani Nandy alivalia gauni jeupe lenye nakshi za kumeremeta huku bwana harusi akiwa amevalia suti ya mtindo wa tuxedo huku wengi wakisubiria kuona mionekano ya wawili hao watakapowasili ukumbini, Mlimani City.