Biashara United yaondolewa kombe la shirikisho

0
3483

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeiondoa timu ya Biashara United ya Tanzania katika mashindano ya kombe la Shirikisho kwa kutofika uwanjani kwenye mechi dhidi ya Ahly Tripoli ya Libya.

Uamuzi wa CAF wa kuiondoa Biashara United kwenye mashindano hayo umefanywa na kamati ya mashindano ya Shirikisho hilo baada ya kubaini kuwa sababu za timu hiyo kushindwa kwenda Libya kucheza mechi hiyo ya hatua ya pili ya raundi ya awali hazikutokana na dharura.
 
Mechi hiyo ilikuwa ichezwe  Oktoba 23 mwaka huu jijini Benghazi nchini Liby