Mshambuliaji mahiri wa Klabu ya Real Madrid Karim Benzema ameibuka kinara katika mchezo wa ligi ya Uhispania maarufu kama La Liga baada ya kufunga mabao 2 ya ushindi dhidi ya Athletic Bilbao.
Katika mchezo huo, Real Madrid walikuwa wa kwanza kupata bao kutoka kwa Toni Kroos katika dakika ya 45 kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Katika kipindi cha pili cha mchezo huo, Ander Capa aliipatia Bilbao goli la kusawazisha lakini magoli mawili ya Karim Benzema yakatosha kuipa Real Madrid ushindi wa mabao 3 kwa 1 dhidi ya Athletic Bilbao.
Usiku wa leo katika uwanja wa Camp Nou, FC Barcelona watawakaribisha vinara wa ligi hiyo Real Sociedad ambao wanaongoza kwa alama 26 baada ya kucheza michezo 13.
Barcelona wapo nafasi ya 8 wakiwa na alama 17 baada ya kucheza michezo 11.