Ben Pol ataja Wanamuziki 15 anaowaona ni bora

0
1674

Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mwigizaji nchini Benard Paul maarufu kama Ben Pol, ametoa orodha ya Wasanii 15 wa muziki ambao kwake anaamini ni bora katika kipindi cha miaka Ishirini iliyopita.

Ben Pol ametoa orodha hiyo kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa twitter ambapo amemuweka Marehemu Albert Mangwea(Ngwair )katika nafasi ya kwanza.

Ben Pol anayeimba zaidi miondoko ya RnB, alianza kuvuma katika muziki mwaka 2010 baada ya kutoa kibao chake cha Nikikupata, ambacho kiliweza kumtambulisha katika ulimwengu wa Bongo Flava.

Nyimbo nyingine ni
Samboira, Moyo Mashine, Jikubali, Namba One Fan, Tatu na Sophia.