Msanii wa Bongofleva Ben Pol ameomba radhi kupitia ukurasa wake wa Instagram kutokana na maneno aliyoyasema kuhusu ndoa yake, wakati wa mfululizo wa mahojiano maalum na mtangazaji MillardAyo yaliyoanza kutangazwa tarehe 13 mwezi huu.
Wakati wa mahojiano hayo Ben Pol alisema hakuifurahia ndoa yake kama alivyotarajia na kukiri kuwa hali ilikua tofauti na jinsi watu wengi walivyokuwa wakitafsiri kupitia picha mbalimbali alizokuwa akiziweka mtandaoni.
Katika chapisho lake la kuomba radhi Ben Pol amesema
“Nia yangu haikuwa kuumiza bali kuwashirikisha juu ya uzoefu wangu ndani ya ndoa na nitalibeba jukumu hili kikamilifu, pia nilitaka kueleza jinsi ilivyoathiri afya yangu ya akili, hata hivyo ninatambua kwamba maneno yangu yalimuumiza mke wangu wa zamani na ninaomba msamaha kwake na kwa umma.”
“Yani sisi sana sana naweza nikasema ilikua ni kaa hapo upige picha, paa paa weka nini……., sisemi kwa ubaya na wala sipo hapa kwa ajili ya kumpeleka mtu mwingine chini ila tu kwa mtazamo wangu mimi naona kama niliingia kwenye picha kuleta ule ukamilifu.”