Anjella kuja na EP

0
6104

First Lady kutoka Konde Gang, Anjella ameatusanua kuwepo na ujio wa EP yake itakayotoka baada ya mwezi mtukufu kumalizika akiwa na lengo na kuwapoza mashabiki zake.

Hata hivyo msanii huyo anayefanya vizuri na ngoma yake ya shulala kwenye msimamo wa TOP20 ya TBC FM amewapongeza mashabiki zake kwa kumuunga mkono Tangu alivyoanza game.

Katika Mahojiano aliyoyafanya na TBC FM kupitia mtaa wa TOP20 amekanusha kununua ‘views’ katika kazi anazozitoa pindi video zinapofanya vizuri kutazamwa na watu wengi katika mtandao wa YouTube kama ilivyotokea hivi karibuni kwa video yake kufikisha watazamaji million mbili.

Anjella amewahadi mashabiki wake baada ya kutoa EP zitafua video na baadaye kazi moja baada ya nyingine huku suala la kutoa albamu likikosa majibu.