Ali Kiba sasa mwendo na Unforgettable Tour

0
1885

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Tanzania, Ali Saleh Kiba  a.k.a King Kiba, amezindua rasmi ziara yake inayojulikana kama Unforgettable Tour, ikiwa ni zawadi kwa Mashabiki wake baada ya safari ya miaka 17 katika muziki.


Katika ujumbe wake kwa Mashabiki wake wa muziki alioutoa kupitia kwa Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, King Kiba amesema kuwa ziara hiyo inatumika pia kuwajengea uwezo Wanafunzi wa Vyuo Vikuu villivyopo kwenye maeneo atakayopita.


Wakati wa ziara hiyo ya Kimuziki, Mwanakuziki huyo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, watakua wakanda kambi kwa ajili ya masuala ya afya ili kuwasaidia wenye matatizo ya kiafya kupata huduma.


King Kiba ametumia uzinduzi wa ziara hiyo maarufu kama Unforgettable Tour akimaanisha kuwa siyo ziara itakayokuja kusahaulika, kutangaza rasmi kuingia mkataba na Msanii Tommy Flavour chini ya lebo yake ya muziki, Kings Music.

Hakusita kuweka hadharani jibu la swali ambalo limekuwa gumzo la kwanini hatashiriki Tamasha la Wasafi kwa kusema kuwa, yeye kama Mwanamuziki ana mambo yake ya kufanya wakati huu ambayo anatarajia yatakua na manufaa kwake siku za baadaye.

Amesisitiza kuwa yeye na Mwanamuziki Diamond Platnumz  hawana Ugomvi wowote na amempongeza kwa mafanikio aliyoyapaya katika Muziki hadl hivi sasa.