AKA auawa kwa risasi Afrika Kusini

0
486

Rapa AKA wa Afrika Kusini amefariki dunia kwa kupigwa risasi muda mfupi kabla ya kutumbuiza jijini Durban.

AKA ambaye jina lake halisi ni Kiernan Forbes ameuawa kwa kufyatuliwa risasi kutoka kwenye gari akiwa amesimama nje ya mgahawa.

Polisi nchini humo wamethibitisha kuwa nyota huyo mwenye miaka 35 pamoja na mlinzi wake wameuawa.

Hajafahamika sababu ya mauaji hayo, na sasa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi.