17 kuwania taji la Miss Ilala 2021

0
2601

Warembo 17 wanatarajiwa kuingia kambini kujiandaa na shindano la urembo la Miss Ilala ambapo mshindi atawakilisha mkoa huo katika shindano la kumtafuta mrembo wa Tanzania.

Mwenyekiti wa kamati ya Miss Ilala Lucas Rutainurwa amewaeleza Waandishi wa habari mkoani Dar es salaam kuwa, mwaka huu wanaanza maandalizi mapema na wana imani kuwa watapata mrembo bora wa kushinda taji la miss Tanzania.

Shindano la kumsaka mrembo wa Ilala linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu ambapo warembo 17 wanatarajiwa kuwania taji hilo mwaka huu.