Wakulima kupata unafuu kununua magari chapa ya Isuzu

0
508

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey Kasekenya ameitaka kampuni ya Almansour Tanzania inayouza Magari chapa ya Isuzu, kuwauzia Wakulima magari hayo kwa bei nafuu ili kuwapunguzia adha ya usafirishaji wa mazao yao kutoka shambani.

Mhandisi Kasekenya ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa bidhaa za magari chapa ya Isuzu ambazo zilizopotea katika soko la Tanzania.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Isuzu Afrika Mashariki Rita Kavashe amesema kampuni hiyo kwa kushirikiana na Kampuni washirika ya Almansour , wana mpango wa kuingia makubaliano na benki mbalimbali ili kuwawezesha Wakulima kupata mikopo kwa ajili ya kununua magari hayo.