Wafanya udanganyifu kwenye matumizi ya maziwa

0
238

Bodi ya Maziwa nchini kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa kipolisi wa Temeke wamebaini uwepo wa tani tatu za maziwa ,yanayokaribia kuisha muda wake wa matumizi, kuongezewa muda huo.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Nchini Noel Byamungu amesema wamebaini kitendo hicho katika kiwanda cha Hawai Limited Kilichopo jijini Dar es Salaam.

Maziwa hayo yalitakiwa kumaliza muda wake wa matumizi katika miezi ya June, Agosti na Oktoba mwaka huu, lakini kiwanda hicho kilifanya kitendo cha Kuyafunga katika vifungashio vipya vinavyoonesha maziwa hayo yataendelea kutumika hadi mwezi Agosti mwaka 2022.