Uzinduzi wa jukwaa la biashara Tanzania – Italia

0
2113

Jukwaa la biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Italia kwa upande wa Tanzania Bara limezinduliwa rasmi leo na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo balozi wa Tanzania nchini Italia, Mahmoud Thabit Kombo amewahimiza Watanzania kuchangamkia fursa zinazoletwa na Serikali, akitolea mfano wa fursa zinazopatikani katika sekta ya utalii kupitia filamu ya The Royal Tour.

Amewahimiza watanzania kujitokeza kwa wingi kufanya biashara na kampuni za nje hasa za kutoka nchini Italia.

Balozi Mahmoud Thabit Kombo ameongeza kuwa biashara hizo zinaweza kufanyika kupitia sekta ya kilimo, uvuvi na utalii.

Kwa upande wake Balozi wa Italia nchini Tanzania Marco Lumbardi amesema hadi sasa miradi yenye thamani ya dola bilioni mbili za kimarekani imewekezwa hapa nchini na kampuni kutoka nchini huko.

Amesema kwa sasa wawekezaji kutoka Italia wamekuja nchini kuangalia fursa zingine zinazopatikana, ili kuendeleza uwekezaji.