Utaratibu waandaliwa kupata takwimu za mazao

0
453

Waziri  wa  Kilimo, -Japhet  Hasunga  amesema kuwa serikali imeandaa utaratibu utakaowezesha kupata takwimu sahihi za uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara, lengo likiwa ni kuratibu soko la uhakika katika ushindani wa mazao.

Hasunga ameyasema hayo mkoani Songwe wakati wa kukagua  shamba la mkulima mkubwa wa zao la kahawa ambaye ni kampuni ya Kanji Lanji lililopo wilayani Mbozi na kuongeza kuwa takwimu zisizo sahihi hudumaza soko la mkulima.

Waziri  huyo wa kilimo ambaye pia ni mbunge  wa  jimbo  la  Vwawa wilayani Mbozi amesema kuwa ni wajibu wa wataalamu wa  Idara ya Kilimo nchini kutayarisha takwimu sahihi za uzalishaji wa mazao ya kilimo na biashara katika maeneo yao.

Amefafanua kuwa takwimu hizo zitaiwezesha serikali kuratibu changamoto zinazojitokeza wakati wa kuuza mazao ya wakulima katika soko la ushindani.