Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa atakutana na Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni kwa lengo la kutia saini makubaliano ya kina ya kibiashra kati ya nchi hizo.
Trump ametoa kauli hiyo jijini Washington baada ya mazungumzo yake na Makamu wa Waziri Mkuu wa China, – Liu He, mazungumzo yaliyohusu masuala ya kibiashara baina ya mataifa hayo mawili.
Amesema kuwa ana imani kuwa mataifa hayo mawili yenye nguvu zaidi za kiuchumi duniani yatafikia makubaliano ya kibiashara ambayo ameyaita kuwa ni makubwa zaidi kuwahi kufikiwa.