Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya mapato ya Serikali ya Shilingi Trilioni 1.767 katika kipindi cha mwezi Septemba pekee.
Kamishna Mkuu wa TRA Dkt Edwin Mhede amesema kuwa, makusanyo hayo ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.20 ya lengo la kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 1.817 katika kipindi cha mwezi Septemba mwaka huu, hayajawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa Mamlaka hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Dkt Mhede kwa vyombo vya habari, ufanisi huo wa mwezi Septemba mwaka huu katika ukusanyaji mapato ya Serikali, ni muendelezo wa ongezeko la makusanyo tangu mwaka wa fedha wa 2019/2020 ulivyoanza mwezi Julai mwaka huu.