Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amewataka wafanyabiashara mkoani humo kujenga tabia ya kulipa kodi kwa hiari na kuwatahadharisha baadhi ya maafisa wa Mamlaka ya Mapato nchini -TRA wanaotumia mianya ya kujinufaisha kwa kuchukua fedha nje ya utaratibu wa serikali kuacha mara moja.
Chalamila ametoa rai hiyo Mkoani Mbeya baada ya kuzungumza na baadhi ya wawekezaji na wafanyabiashara kuhusiana na changamoto zinazowakabili na namna ya kuzitatua.
Amesema moja ya mikakati ya uongozi wa Mkoa wa Mbeya ni kuhakikisha wawekezaji wanajengewa uwezo na mazingira mazuri ili waweze kulipa kodi.
Ameongeza kuwa lazima kuwepo na mahusiano ya moja kwa moja kati ya mfanyabiashara na serikali yatakayowezesha kwa pamoja kufikia malengo ya kuinua uchumi nchini.