TIC yamaliza mgogoro baina ya mwekezaji na TRA Kagera

0
1045
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC Godfrey Mwambe akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha Pombe kali cha Ambiance cha Mkoani Kagera wakati alipofanya ziara kiwandani hapo hivi karibuni

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geoffrey Mwambe akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenera Marco Gaguti wamefanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha vinywaji Vikali cha Ambiance Distilleries Tanzania Ltd kwa lengo la kumaliza mgogoro baina ya kiwanda hicho na Mamlaka ya mapato Tanzania –TRA sambamba na kukirejesha kiwanda hicho katika  uzalishaji.

Baada ya mazungumzo, TRA na kampuni ya Ambiance  kukubaliana kwamba kodi ya ushuru wa ndani iliyokuwa ikidaiwa na TRA kwa mujibu wa sheria takribani Tshs. milioni 500  italipwa na kampuni kwa awamu,  tofauti na ilivyokuwa ikitakiwa awali kulipwa mara moja jambo  lililoonekana kuwa kikwazo kwa kampuni. Vilevile  baada ya makubaliano hayo, kampuni  imeahidi kuendelea na uzalishaji wake pamoja na maandalizi ya upanuzi wa mradi huo ikiwamo kisimika mitambo ya kuzalisha chupa za vinywaji badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi.

Kufikiwa kwa makubaliano hayo ni hatua ya mafanikio kwa TIC ikizingatiwa kwamba mradi una faida kwa Mkoa na Taifa ikiwamo kodi, ajira kwa vijana, hamasa kwa wawekezaji wengine wa viwanda kuwekeza koani Kagera na kuongeza pato la Taifa.

Mwambe anawakaribisha wawekezaji wenye changamoto kufika TIC ambabyo ipo tayari kushughulikia changamoto za uwekezaji dhidi ya mammlaka mbalimbali ili kufanikisha uwekezaji nchini.

Story by. James Range