Kampuni ya Microsoft inayojishughulisha na utengenezaji wa programu za kompyuta, inatarajia kusitisha kuuza leseni za Windows 10 mwishoni mwa nwezi huu.
Kwenye ukurasa rasmi wa “PC World” imetangazwa ifikapo Januari 31, 2023 itakuwa ni siku ya mwisho ya kununua na kupakua matoleo ya programu ya Windows 10 Pro.
Ni wazi kwamba Microsoft inaendelea kuachana kutoa Sasisho (Updates/ Support) kwa Windows 10 kutokana na mpango wake wa kuachana na programu hiyo ifikapo mwezi Oktoba mwaka 2025 kulingana na taarifa zilizokwishatolewa hapo awali na kampuni hiyo ya Microsoft.
Hata hivyo kampuni ya Microsoft kwa sasa itaendela na utaratibu wa kutoa sasisho (Updates/Support) ya Windows 10 ambayo itakuwa inahusu usalama wa kompyuta ili kusaidia kulinda kompyuta dhidi ya virusi, vidadisi na programu zingine vamizi wa taarifa hadi ufikapo mwezi huo wa Oktoba, 2025 itakapokuwa imefikia kikomo rasmi cha kutoa sasisho hizo.
Utaratibu huo utatekelezwa kwa upande wa kampuni ya Microsoft ila mtumiaji wa kompyuta anaweza kununua leseni za Windows 10 kutoka kwa wauzaji wengine wa rejareja kama vile Amazon na Newegg ikiwa bado programu hizo hazijawaishia.
Aidha kwa kompyuta mpya zitazoendelea kuuzwa zitakuja na programu ya windows 11 tayari kwa matumizi.