Microsoft kukabiliana na itikadi za kigaidi mitandaoni

0
1414

Kampuni ya Microsoft imekuja na mpango kabambe wa kuondoa maudhui yenye viashiria vya ugaidi na vurugu mitandaoni.

Mpango huo ni sehemu yao ya kazi ya kuendeleza utumiaji wa teknolojia bandia (AI) ambao unalenga katika kuwawezesha watafiti, kuongeza uwazi na kukuza ulinzi kupitia akili bandia (AI).

Kupitia mpango huu Microsoft imeweka ahadi ya dola laki tano kufadhili utafiti wa teknolojia za kuimarisha faragha na athari za kijamii zinazosababishwa na ‘search engines’ zinazoendeshwa na Teknolojia bandia (AI)

Rais wa Microsoft kupitia ukurasa wa kampuni hiyo ameeleza kuwa katika kuwawezesha watafiti, wanajiunga na mitandao ya kijamii kama Twitter na Serikali ya Newsland na Marekani ili kutafiti zaidi athari za mifumo ya teknolojia bandia inayopendekeza maundui mtandaoni.

Aidha, katika kipengele cha kukuza uwazi amesema kuwa wanachukua hatua zaidi kuongeza uwazi na udhibiti wa watumiaji wa mifumo iliyotengenezwa na Microsoft na kutaja mifumo hiyo kuwa ni LinkedIn na Azure Personalizer.