iphone 14 kupiga simu za dharura kupitia setilaiti

0
2290

Kampuni ya Apple imewekeza teknolojia mpya ya kupiga simu za dharura “emegency call” kupitia setilaiti katika toleo jipya la simu ya iphone 14 ambayo imezinduliwa na kuwekwa sokoni siku ya jana.

Mchambuzi Mkuu wa kampuni ya kimataifa ya tafiti na ushauri wa masuala ya teknolojia, CCS Insight Ben Wood ameiambia tovuti moja kuwa, uwekezaji huo wa kuwezesha mawasiliano ya simu za dharura kufanyika kupitia setilaiti utasaidia kupatikana kwa taarifa za dharura kupitia mawasiliano yenye uhakika.

Ameongeza kusema juhudi zilizofanyika ili kufanikisha teknolojia hiyo ni pamoja na kuingia makubaliano ya kibiashara kati ya kampuni hiyo ya Apple na mtoa huduma za Setilaiti, Globalstar pamoja na kuunda miundombinu inayohitajika kupitisha ujumbe wa simu wa huduma hizo za dharura.