Microsoft imetangaza kuwa Februari 14, 2023 itakifuta rasmi kivinjari cha Internet Explorer kutoka katika kompyuta za watumiaji duniani kote.
Kampuni ya kiteknolojia ya Microsoft kwa awamu imekuwa ikiiondoa sokoni bidhaa yake ya Internet Explorer 11 tangu Juni 15 mwaka huu huku programu hiyo ikiwa imedumu kwa takribani miaka 30 sasa.
Sasa ni rasmi kuwa Februari 14 ambayo hutambulika kama siku ya wapendanao itakuwa ndio mwisho wa kivinjari hicho.
Watumiaji wa kivinjari hicho wataona maboresho ya Microsoft Edge ambayo ndiyo yatakayokifuta kabisa kivinjari hicho katika baadhi ya vifaa vya Windows 10
Kampuni ya Microsoft imeandika tangazo kupitia ukurasa wake lililosomeka kuwa “Programu ya kompyuta ya Internet Explorer 11 (IE11) imepangwa kuzimwa kabisa kwenye baadhi ya matoleo ya vifaa windows 10 mnamo Februari 14, 2023, kupitia maboresho ya Microsoft Edge.”