Tanzania yashiriki maonesho ya biashara Comoro

0
3784

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeratibu na kufanikisha kampuni 15 nchini kushiriki maonesho ya kimataifa ya biashara katika mji wa Moroni nchini Comoro.

Msafara huo wa wafanyabiashara umeratibiwa na Tantrade kwa kushirikiana na ubalozi wa Tanzania nchini Comoro.

Maonesho hayo ya biashara na huduma kwa bidhaa kutoka Tanzania yaliyanza tarehe 8 mwezi huu na yanatarajiwa kufikia tamati hii leo.

Bidhaa zilizowasilishwa na Tanzania katika maonesho hayo pamoja na kahawa, matunda, asali, nyama, vinywaji, vifaa vya umeme, magodoro na samani.