Taasisi zatakiwa kuchangia elimu

0
1205

Benki na taasisi mbalimbali zinazojihusisha na utoaji wa misaada nchini zimehimizwa kusaidia kuboresha sekta ya elimu katika maeneo yao, ikiwa ni moja ya jitihada za kuiunga mkono serikali ambayo imekua mstari wa mbele katika kuboresha sekta hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke mkoani Dar es salaam, -Lusibilo Mwakabibi  katika shule ya msingi ya Mabatini baada ya kupokea msaada wa mabati na Kompyuta kutoka benki ya NMB.

Msaada   huo una thamani  ya zaidi ya shilingi milioni 15 na umetolewa kwa shule Nne za Manispaa ya Temeke ambazo ni Azimio, Tandika, Mabatini na Karume.