Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dkt Bernard Kibesse, amezitaka Taasisi za Kibenki kutoa huduma bora zenye ushindani ili kuinua uchumi wa Taifa.
Naibu Gavana Kibesse ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati akizindua tawi jipya la Benki ya Exim la Mkwepu, ambalo awali lilikuwa chini ya Benki ya UBL kabla ya kununuliwa na Benki ya Exim.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Tanzania, -Jaffari Matundu amesema kuwa, Benki hiyo itaendelea kuimarisha huduma zake nchini ikiwa ni pamoja na kuongeza matawi na kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wateja wake.
Benki ya Exim ilianzishwa miaka 22 iliyopita, ambapo mpaka sasa ina matawi 33 nchi Tanzania.