Soko la hisa nchini China limeshuka kwa asilimia Tano, kiwango ambacho kinaonekana kuwa ni kikubwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Wachunguzi wa masuala ya biashara wamesema kuwa mgogoro wa kibiashara kati ya China na Marekani huenda umechangia kushuka kwa soko hilo.
Habari zaidi kutoka nchini China zinasema kuwa kushuka kwa soko la hisa la nchi hiyo kunaweza kuathiri uchumi wa Taifa hilo kubwa kiuchumi.