Shindano la wazalishaji wa viwandani lazinduliwa Dar es Salaam

0
308

Wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini kupitia viwanda vidogo na kati wamehimizwa kujitokeza kushiriki mashindano ya 15 ya tuzo za Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ili kuitangaza Tanzania kimataifa.


Akizindua mashindano hayo Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Leodegar Tenga amesema, lengo la mashindano hayo ni kukuza uchumi wa nchi kupitia viwanda vidogo na Kati kwa kutumia malighafi zinazopatikana nchini.

Tenga ameongeza kuwa uzinduzi wa shindano hilo unafungua milango kwa wadau mbalimbali kwenye sekta ya viwanda kujisajili ili kushiriki kabla ya Oktoba 12, 2020.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa tuzo hizo akiwemo Meneja wa Masoko na Mauzo Kampuni ya Plasco Limited, Edith James, wamesema mashindano hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza soko la bidhaa zinazozalishwa nchini.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu ambapo Rais Dkt. John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.