Probox marufuku kubeba abiria Kigoma

0
3617

Serikali mkoani Kigoma imepiga marufuku magari madogo aina ya Probox maarufu kama michomoko na wish kufanya Kazi za kukusanya abiria kwenye vituo kama daladala.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema magari hayo yamesajiriwa kupakia abiria kwa utaratibu wa kukodishwa na si kukusanya abiria barabarani kama daladala.

Aidha amelitaka jeshi la polisi mkoani humo kufuatilia suala hilo Ili madereva wa magari hayo watakaokiuka utaratibu kuchukuliwa hatua za kisheria.