Mtanzania apata madini ya Tanzanite ya bilioni 7.8

0
1033

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila amesema kuwa leo wizara inamtabua mchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite, Saninniu Laizer kuwa bilionea baada ya kupata mawe makubwa mawili yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8.

Mchimbaji huyo amepata mawe hayo mawili ambapo moja lina kilo 9.2 ambalo thamani yake ni shilingi bilioni 4.5 na la pili lina kilo 5.8 lenye thamani shilingi bilioni 3.3.

“Na utofauti wake ni kwamba mawe ya uzito huo hayajawahi kupatikana kwenye machimbo ya Tanzanite tangu machimbo yaanze na yamepatikana ndani ya ukuta wa Mirereni kwahiyo hii ni rekodi mpya ya kupata mawe yenye uzito huo,” amesema Prof. Msanjila.

Profesa Msanjila amesema kuwa sekta ya madini inauwezo wa kumfanya mtu kuwa bilionea kwa haraka, ameongeza kuwa kunahitaji kuwa uwekezaji wa dhati katika sekta hiyo.