Msemaji wa Soko la Hisa la Dar es Salaam Mary Kinabo
Wiki iliyopita ilikuwa yenye mavuno manono kwa soko la hisa la Dar es salaam (DSE) baada ya mauzo ya hisa kuongezeka karibu mara nne ikilinganishwa na mauzo ya hisa ya wiki iliyoishia Januari 11.
Kwa mujibu wa taarifa ya Soko hilo, mauzo ya hisa yaliongezeka na kufikia shilingi bilioni 1.8 wiki iliyopita kutoka shilingi milioni 371 katika wiki iliyotangulia kutokana na kupanda kwa bei za hisa za kampuni mbalimbali zikiwemo DSE wenyewe na benki ya CRDB.
Msemaji wa soko hilo Mary Kinabo amesema mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa katika soko la hisa la Dar es salaam pia umeongezeka kwa shilingi bilioni 16.