Kongani ya viwanda 200 kujengwa Kibaha

0
6550

Tanzania inaenda kuandika historia nyingine kwenye sekta ya uwekezaji wa viwanda kwa kuwa na kongani kubwa ya viwanda 200 katika eneo la Kwala, Kibaha mkoani Pwani.

Mradi huo ambao leo mwekezaji kutoka China, Kampuni ya SINO TAN INDUSTRIAL PARK amekabidhiwa ardhi yenye ukubwa wa Ekari 2500 unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu.

Akizungumza baada ya kushuhudia makabidhiano rasmi ya ardhi kwa mwekezaji wa mradi huo unaogharimu Dola za Marekani bilioni 3, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji anasema uwekezaji huo unaenda kusaidia serikali kupunguza matumizi ya fedha ya kigeni kuagiza bidhaa kwa kiasi kikubwa.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Prof. Godious Kahyarara mradi huo unatarajiwa kutoa ajira za moja kwa moja 100,000 na zisizo za moja kwa moja 300,000.