iPhone 12 yaiteka mitandao ya kijamii

0
421

Kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Apple, maarufu kwa simu za iPhone na tarakalishi zake za Mac imetambulisha simu mpya aina ya iPhone 12 zinazozungumziwa zaidi mitandaoni.

Toleo jipya la iPhone 12 lina aina tatu za simu (iPhone 12, iPhone 12 Mini na iPhone 12 Pro) ambazo zina muonekano wa nje wa kufanana na toleo lao la zamani la iPhone 5.

iPhone 12 Mini ambayo inatofautiana kidogo na iPhone 5 kwa ukubwa lakini nyembamba zaidi ndio simu ndogo itayokuwa na uwezo mkubwa zaidi ikiwemo kuwa na 5G.

Simu hizo zitaanza kuuzwa kuanzia Novemba mwaka huu huku bei ikianzia chini (TZS milioni 1.6) tofauti na ilivyodhaniwa kwamba ingekuwa na bei zaidi ya iPhone 11.

Tofauti na matoleo yaliyopita ya iPhone 5, 6,7,8, X, na 11, iPhone 12 imekuja na chaji ya sumaku (isiyotumia waya) inayochajia yuma ya simu.