Mwenyekiti wa sekta Binafsi hapa nchini –TPSF Salum Shamte amesema, serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli inafanya vizuri katika kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara hapa nchini.
Akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa maonesho ya 4 ya Viwanda yanayofanyika Jijini Dar es salaam, Shamte amesema, Mpango wa kufanya biashara “Blue Print” utasaidia kurahisiha mazingira ya kufanyia biashara hapa nchini.
Akisoma taarifa ya Taasisi ya Sekta Binafsi hapa nchini Shamte amesema, kwa sasa mazingira ya kufanya biashara yanazidi kuimarika na hivyo kupunguza urasimu na Rushwa uliokuwa ukikwamisha kukua kwa uchumi.
Story by. James Range