Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, imetangaza kugawa faida ya Shilingi Bilioni 2.5 kwa Wateja na Mawakala wake wanaotumia huduma ya Airtel Money baada ya kupata kibali kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Faida inayotokana na Airtel Money, ni fedha ambayo Airtel imekuwa ikiirudisha kwa Wateja wake waliotumia Airtel Money kwa kila robo ya mwaka kulingana na kiwango ambacho kipo kwenye akaunti zao za Airtel Money kila siku.
Mkurugenzi wa Airtel Money, -Isack Nchunda amesema kuwa Mteja atatumiwa faida yake kwenye akaunti yake ya Airtel Money na anaweza kuamua kuzitoa, kutuma au kuzitumia kwa matumizi yoyote ikiwemo kulipia bili mbalimbali.
Nchunda amesisitiza kuwa, faida itokanayo na matumizi ya Airtel Money itagawiwa kwa Wateja wa Airtel Money na Mawakala wote nchini ambao wametumia huduma hiyo kwa muda wa miezi 12 iliyopita.
Hii ni mara ya Nane kwa Airtel kutoa faida kwa Wateja wake wote wa Airtel Money tangu mwaka 2015.
Mpaka sasa, jumla ya Shilingi Bilioni 19 zimetolewa kama faida kwa Wateja na Mawakala wote nchini.