Bidhaa ziongezwe thamani

0
481

Esther Maruma, ambaye ni miongoni mwa wachangia mada katika mjadala unaohusu mabadiliko ya uchumi duniani, athari na suluhisho kwa Mwananchi wa kawaida amesema, katika kipindi hiki cha mdororo wa kiuchumi Duniani Taasisi za fedha zinapaswa kuangalia maeneo ambayo yatasaidia nchi kuendelea kukua kiuchumi.

Ametaja maeneo hayo kuwa ni pamoja na kuboresha biashara kwa kuongeza thamani kwa bidhaa zinazozalishwa ndani ya nchi ili ziweze kuuzwa nje.

Maruma ameongeza kuwa sekta ya kilimo ina mchango mkubwa katika kuongeza pato la Taifa, japo watu wengi kwa sasa wanalima kwa lengo la kupata chakula na wachache ndio hufanya kilimo biashara.

Amesema mazao ya kilimo yakiongezwa thamani kwa kuchakata bidhaa hizo yanaweza kuchangia maradufu katika pato la Taifa.

Mjadala huo kuhusu mabadiliko ya kiuchumi duniani, athari zake na suluhisho kwa taasisi na Mwananchi wa kawaida umeandaliwa na Taasisi ya Wakurugenzi Tanzania (IoDT) na kudhaminiwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
na kampuni nyingine.