Bibi anayefanya biashara ya kupiga picha Iringa kumlea mjukuu

Ujasiriamali

0
3298

Mpigapicha mwenye miaka 60, Flora Kanagwe kutoka mkoani Iringa amesema amelazimika kufanya kazi hiyo ili kumudu maisha ya kumlea mjukuu wake mwenye ulemavu.

Flora anapiga picha mtaani huku akimbeba mjukuu wake mgongoni kwa kuwa hana mtu wa kumwacha nae nyumbani.

Kazi hiyo inamwingizia shilingi 20,000 kwa siku.

Wateja wake wanaifurahia kazi yake na kusema ni mwaminifu kuliko wapigapicha vijana wengi.