Benki 23 zafutiwa leseni Ghana

0
1380

Maelfu ya Raia wa Ghana ambao wameweka akiba zao katika benki mbalimbaliza nchi hiyo, wamepata wasiwasi wa kupoteza akiba hizo kufuatia hatua ya

Banki Kuu ya nchi hiyo kufuta leseni 23 za benki pamoja na taasisi nyingineza kifedha.

Benki Kuu ya Ghana imefuta leseni hizo kwa madai kuwa, hazina mtaji wakutosha kwa ajili ya kujiendesha.

Habari kutoka nchini Ghana zinasema kuwa, takribani watu Elfu Sabini wameathiriwa na hatua hiyo ya Benki Kuu, baada kuweka akiba zenye thamani ya Dola Bilioni Moja Nukta Sita za Kimarekani kwenye benki hizo.

Benki Kuu ya Ghana imezishutumu Benki zilizofutiwa leseni kwa kutofanyakazi zao kwa ufanisi, hali iliyosababisha kukosa mtaji.

Hata hivyo baadhi ya watumiaji wa benki nchini Ghana wamesema kuwa,

Benki Kuu ya nchi hiyo ndiyo inapaswa kulaumiwa kwa kutokua makini katika usimamizi, na hivyo kuzifanya benki hizo kujiendesha bila kufuata masharti kwa muda mrefu.