ATCL yazindua safari kutoka Dar es salaam kwenda Geita

0
259

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), leo imezindua rasmi safari za ndege kutoka Dar es salaam kwenda mkoani Geita na kutoka Geita kwenda Dar es salaam.

Kwa kuanzia, ATCL wataanza safari mara mbili kwa wiki siku za Jumamosi na Alhamisi.

Kuanzia tarehe 18 mwezi huu safari hizo zitaongezwa na kuwa mara tatu kwa wiki katika siku za Jumatatu, Alhamisi na Jumamosi.