Serikali kushirikiana na wadau kuboresha sekta ya afya

0
141

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ameushukuru uongozi wa Shirika la Afya la Japan
(Tokushukai Medical Group), kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kupitia hospitali ya Benjamin Mkapa kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.

Dkt. Mollel ametoa shukrani hizo alipokutana na uongozi wa shirika hilo katika ofisi za wizara ya Afya jijini Dodoma.

“Ninawashukuru kwa namna mlivyoungana na hospitali ya Benjamin Mkapa na chuo Kikuu cha Dodoma, nchi ya Japan imekuwa ikisaidia katika kuboresha sekta ya afya kwa kuhakikisha huduma zinapatikana hasa katika matibabu ya figo. ” amesema Dkt. Mollel

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Benjamin Mkapa Dkt. Alphonce Chandika amesema shirika hilo la Afya la Japan limekuwa likitoa msaada mkubwa kwa hospitali hiyo.

Naye mwenyekiti wa Shirika hilo la Afya la Japan Profesa Higashiue Shinichi ameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha sekta ya afya.