Sababu za watu kunenepa haraka kuliko wengine

0
253

Kwa mujibu wa tafiti mpya iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Copenhagen, imeelezwa kuwa baadhi ya watu wana aina fulani ya vijidudu katika utumbo ambavyo hufanya kazi ya kuvuna virutubisho kwa wingi na ubora zaidi kulinganisha na wengine.

Hii inaweza kuwa ni hatua muhimu itayopelekea kuelewa ni kwanini watu wengine hunenepa kwa urahisi zaidi kuliko wengine angali wanakula sawa.

“Huenda tumepata ufunguo wa kuelewa kwa nini baadhi ya watu hupata uzito zaidi kuliko wengine, hata wakati wanakula kiasi sawa cha chakula. Lakini hili linahitaji kuchunguzwa zaidi,” anasema Profesa Mshiriki Henrik Roager wa Idara ya Chuo Kikuu cha Copenhagen cha Lishe, Mazoezi na Michezo.

UTAFUTI KWENYE KINYESI

Watafiti walichunguza virutubisho vilivyobaki kwenye kinyesi cha mtu afahamikaye kama Danes (85) ili kutathmini ufanisi wa vijidudu hivyo katika kunyonya nishati kutoka kwenye chakula.

Kulingana na matokeo ya zoezi hilo, takribani asilimia 40 ya washiriki ni wa kundi ambalo kwa wastani wana uwezo wa kupata virutubisho zaidi kutoka kwenye chakula kuliko hao asilimia 60 nyingine waliobakia.

Watafiti pia waligundua kuwa watu ambao walipata virutubisho vingi kutoka kwenye milo yoa walikuwa na uzito uliozidi kwa asilimia 10 zaidi kwa wastani, ambayo ni sawa na uzito takribani kilo 9

Hivyo tafiti zimeonesha kuwa uzito uliopita kiasi unaweza kuhusishwa na sabahu zaidi ya namna mtu anavyokula chakula bora au kiwango cha mazoezi anachofanya.

UMBALI NA MUDA WA CHAKULA TUMBONI

Watafiti pia wamechunguza muda wa safari ya chakula katika mwili kwa watu ambao wote wana mifumo sawa ya lishe ambapo wakatoa madai kuwa watu ambao chakula huchukua muda mrefu zaidi kusafiri hupata virutubisho zaidi kutoka kwenye lishe zao.

Hata hivyo walibaini zaidi kuwa kwa washiriki waliokuwa bakteria wa tumboni aina ya B ambao kwao chakula huchukua muda mfupi kusafiri na kumeng’enywa, bado walinenepa. Hili liliwafanya waone kuwa, sababu ya kunenepa si muda ambao chakula kinasafiri, bali ni bakteria ndani ya mwili.