Mti huu unaitwa Mlonge (moringa oleifera), asili yake ni uhindi na unapandwa maeneo ya kanda za tropiki na nusutropiki.
Maganda mabichi ya Mlonge, maua yake, mbegu, mizizi na majani yake hutumika kama chakula na dawa kwa binadamu na hata mifugo.
Mti huu una uwezo wa kuponya magonjwa mengi, kama vile; vidonda vya tumbo, malaria, homa ya tumbo, matatizo ya macho, maambukizi ya mfumo wa mkojo na mengine mengi.
Pia mti huu una virutubisho vya omega-3 ambavyo havipatikani katika maziwa na nyama.