Rais John Magufuli amewataka Wafanyabiashara na Wawekezaji nchini kuheshimu sheria na bei elekezi kwa Wazalishaji na kuacha kuwanyonya Wakulima ambao wengi maisha yao ni duni.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati wa kongamano la kwanza la biashara kati ya Tanzania na Uganda.
Pia amewataka Wafanyabaishara wa Tanzania na Uganda kushirikiana na kuagiza vikwazo vilivyokuwa vikizuia ushirikiano kuondolewa.
Rais Magufuli ameongeza kuwa, yeye pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wanasubiri kutekeleza mambo yote yatakayojadiliwa na kufikiwa makubaliano na Wafanyabiashara hao wa Tanzania na Uganda.
Lengo la kongamano hilo la siku Mbili lililofunguliwa na Rais Museveni ni kutangaza fursa na kuhamasisha biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.
Kongamano hilo linafanyika pamoja na maonesho ya bidhaa mbalimbali za Tanzania, ambapo Watanzania wanapata fursa ya kuonesha bidhaa za kilimo na za viwandani.